Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai amerejea kutoka nchini India alikokuwa akifanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.
Mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Mheshimiwa Ndugai alisema kwa sasa afya yake iko imara kabisa na anaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu na Madaktari waliokuwa wakimfanyia uchunguzi Nchini India.
Mhe. Ndugai pia amewashukuru watanzania wote kwa dua na sala zao katika kipindi alichokuwa India ambazo zimemuwezesha kuimarika kwa afya yake na hatimaye kurejea nchini salama.
Mbali na kutoa shukrani hizo Mheshimiwa Ndugai pia amewatakia Watanzania wote kheri na nafaka ya sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.
Sambamba na hilo Mhe Ndugai amewakumbusha pia Waheshimiwa Wabunge kujiandaa na shughuli za Bunge ambazo zinatarajia kuanza hivi karibuni.
Katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere Mhe. Ndugai alilakiwa na Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dkt Tulia Ackson ambaye aliambatana na Viongozi wengine wa kitaifa akiwemo Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Merdad Kaleman, Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura, Mbunge wa Arusha Mjini Mhe. Godbless Lema na Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah.

Watanzania leo wanaelekeza macho na masikio yao mjini Dodoma, kusikiliza Hotuba ya Bajeti ya Serikali, inayotarajiwa kusomwa saa 10 kamili bungeni na Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum.
Tayari Waziri Saada alishaeleza kuwa makadirio ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2014/15, unaoanza Julai mwaka huu, yatakuwa Sh trilioni 19.6 kutoka makadirio ya Sh trilioni 18.2 ya Bajeti inayoisha muda wake.

Vipaumbele vya Bajeti hiyo, kwa maana ya miradi itakayozingatiwa zaidi, ni iliyo katika Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) unaohusisha sekta sita za Kilimo, Elimu, Maji, Utafutaji rasilimali fedha, Nishati, Uchukuzi na Uboreshaji wa Mazingira ya kufanyia biashara na Mpango wa Maendeleo ya Miaka Mitano.

Akisoma mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo kwa mwaka 2014/2015, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Stephen Wassira, alisema mapendekezo ya mpango huo, yana vipaumbele vitano.

Cha kwanza ni miundombinu, kikifuatiwa na kilimo, viwanda vinavyotumia malighafi za ndani na kuongeza thamani, maendeleo ya rasilimali watu na ujuzi na uendelezaji wa shughuli za utalii, biashara na fedha.

Katika hotuba hiyo, Watanzania wengi watakuwa makini kusikiliza bidhaa na huduma zitakazoongezwa kodi, jambo linalotarajiwa kuongeza bei ya bidhaa za huduma husika katika soko.

Katika bajeti inayoishia, Serikali iliongeza kodi kwenye magari makuukuu, bia, vinywaji vikali na baridi ambavyo kodi imekuwa ikiongezwa kila mwaka na kuwaathiri watumiaji.

Kutokana na hali hiyo wanywaji pombe na sigara baada ya bajeti ya mwaka juzi ya 2012/2013, walilazimika kutumia fedha nyingi ili kupata huduma hizo kwa kiwango kile kile katika mwaka huu wa bajeti unaoisha.

Bidhaa zisizokuwa za mafuta ambazo zilifanyiwa marekebisho na kuongezwa kodi ni mvinyo, pombe, vinywaji vikali, na sigara.

Ushuru pia uliongezwa kwenye magari yasiyokuwa ya uzalishaji na yenye umri wa miaka 10 kutoka asilimia 20 mpaka asilimia 25.

Lengo la Serikali katika hilo, lilikuwa kupunguza uagizaji wa magari chakavu ili kulinda mazingira na kupunguza ajali za mara kwa mara.

Katika bajeti hiyo, vijana wa bodaboda walicheka baada ya Serikali kusamehe ushuru wa barabara kwa pikipiki hizo za biashara.

Moja ya kivutio kikubwa cha Bajeti inayowasilishwa leo, ni matarajio ya wafanyakazi kuhusu utekelezaji wa ahadi ya Rais Jakaya Kikwete, aliyoitoa katika sherehe za Mei Mosi mwaka huu, ya kuongeza mshahara wa kima cha chini na kupunguza kodi ya mshahara (PAYE).

Rais Kikwete alisema Serikali itaendelea kuongeza mshahara wa kima cha chini na kubainisha kuwa mwaka 2005 alipoingia madarakani, alikuta mshahara wa kima cha chini ni Sh 65,000 na kukipandisha taratibu hadi kufikia Sh 240,000 cha sasa.

Kuhusu kupunguza PAYE, Rais Kikwete alisema kusudi la Serikali ni kupunguza kodi hiyo ya mshahara kutoka asilimia 13 inayotozwa sasa, ifikie katika kiwango cha tarakimu moja.

Kuhusu misamaha ya kodi ambayo mwaka huu imekuwa gumzo bungeni, huku wabunge wengi wakitaka ipunguzwe, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, alinukuliwa akisema wafanyabiashara na vigogo wanaokwepa kodi kwa kujificha kwenye mwavuli wa misahama, hawako salama.

“Tutafuatilia kikamilifu kwa kuwa wapo watu wanaingiza bidhaa wanapewa msamaha, lakini ukija kwenye huduma za jamii unakuta bidhaa hizo zinauzwa kibiashara,” alisema.

Mwigulu pia alizungumzia ukwepaji kodi na matumizi mabaya ya fedha za Serikali na kufafanua kuwa, yatadhibitiwa.

“Bahati nzuri niliyonayo, sikuzaliwa na chembe ya woga, kwa hiyo kwenye hili hakuna mkubwa wala mdogo, hakuna mtu atagusa fedha ya umma kwa kukwepa au kwa kutumia vibaya kodi ambayo ilishakusanywa halafu akapona asiguswe,” alisema.

Mwigulu alisema katika Bajeti ya Serikali ya 2014/2015, yapo mambo ya msingi matano, ambayo yatasimamiwa kikamilifu ili kuhakikisha utekelezaji wake unakuwa tofauti na zilizopita.

Mbali na kuondoa misamaha ya kodi, pia makusanyo ya ndani yatatiliwa mkazo zaidi ili kujenga uwezo wa kujitegemea wenyewe badala ya kutegemea wahisani.

Jambo la tatu alisema ni kuhakikisha Serikali inapeleka fedha kwenye mahitaji muhimu na kwa wakati, ili fedha za maendeleo zitumike kama ilivyokusudiwa.

Jambo la nne litakalozingatiwa kwa mujibu wa Mwigulu, ni usimamizi wa fedha zinazopatikana kwani pamoja na makusanyo kidogo, lakini pia kuna uvujaji.

“Tunataka fedha inayopatikana na kupangiwa kazi fulani itumike kwa shughuli iliyokusudiwa. Tutahakikisha tunasimamia na kudhibiti matumizi yake,” alisema.

Naibu Waziri huyo wa Fedha alisema eneo la tano ambalo litaangaliwa ni fedha ambazo hazitokani na kodi, bali zinachangwa na wananchi na wadau wengine katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Alisema eneo hilo ni muhimu mbalo Serikali inaona kuna haja ya kulisimamia vizuri, ili kuhakikisha fedha za wananchi zinatumika vizuri.

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, John pombe Magufuli, hii leo kwa mara ya kwanza amelihutubia bunge huku akiahidi kuwa serikali yake itafanya kazi kwa weledi, wakati huu pia akimwapisha waziri mkuu mpya, Majaliwa Kassim Majaliwa.

Ni sauti yake waziri mkuu mpya wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa, wakati akila kiapo hii leo mjini dodoma katika ikulu ndogo ya Chamwino, sherehe ambayo mbali na kuhudhiriwa na rais wa Zanzibar na viongozi wastaafu, wabunge na wageni mbalimbali nao walihudhuria.
Baada ya sherehe za kuapishwa kwa waziri mkuu, baadae wabunge walirejea bungeni ambako rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli aliwahutubia, ikiwa ni mara yake ya kwanza kufanya hivyo toka alipoteuliwa kuwa rais baada ya uchaguzi wa October 25 mwaka huu.
Kwenye hotuba yake rais Magufuli, aliwashukuru wananchi kwa mara nyingine kwa kumuamini na kumchagua, ambapo ameahidi kuwa kiongozi atakayewatumikia watu wote bila kubagua, na kwamba lengo lake ni kuhakikisha nchi ya tanzania inasonga mebel kimaendeleo.
Rais Magufuli pia kwenye hotuba yake pia akaeleza malalamiko aliyoyapokea kwa wananchi ambayo yeye anaona ni kero kwa wananchi, maeneo ambayo anasema ni lazima yashughulikiwe ipasavyo ili kuleta uaminifu kwa wananchi.
Kuhusu Uchumi rais Magufuli amesema kuwa serikali yake itakuwa ni serikali ya viwanda itakayosimamia sheria na kuhakikisha kuwa uchumi wa nchi unasimama kwa kujenga na kuendelea viwanda ili kutengeneza ajira zaidi.
katika hotuba yake pia, rais magufuli hakuacha kugusia suala la katiba mpya, ambapo amesema atahakikisha serikali yake inasimamia mchakato huo na kwamba safari hii utakamilika kwa wakati.
Rais Magufuli pia akagusia suala la muungano pamoja na hali ya kisiasa visiwani zanzibar ambapo amesema yeye ni muumini mkubwa wa muungano uliopo na kwamba anaamini mgogoro wa zanzibar uliojtokeza unatatuliwa kwa amani.
Kabla ya kuanza kwa hotuba yake bungeni, rais Magufuli alishuhudia vioja vya upinzani ambao walikuwa wakipiga kelele wakati viongozi wa zanzibar walipokuwa wakiingia bungeni bungeni, ambapo baadae spika wa bunge Job Ndugai alilazimika kutumia kiti chake kuwafukuza nje ya ukumbi wa bunge ili kupisha hotuba ya rais kuanza, jambo ambalo upinzani ulitii na kutoka nje.

Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah akiongea na na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Aziz Ponary Mlima pamoja na maafisa wa Ubalozi walipotembelea Ubalozi wa Tanzania Jumatatu. Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah pamoja na Maafisa wa Bunge akiwa katika picha ya na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Aziz Ponary Mlima pamoja na maafisa wa Ubalozi walipotembelea Ubalozi wa TanzaniaJumatatu tarehe 02 March 2015.
   
Ofisi ya Bunge imepokea kwa masikitiko taarifa kuhusu tafsiri ya kusitisha matangazo ya Shughuli za Bunge na Kamati, kinyumena jinsi ilivyoakisiwa katika mazungumzo ya pamoja kati ya Wanahabari na Katibuwa Bunge.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa, Bunge la Jamhuri ya Muungano halina mpango wa kusitisha matangazo ya Bunge wala Kamati zake, ambazo kwa mahitaji ya sasa nazo zinapaswa kurushwa moja kwa moja kama sehemu ya mpango kabambe wa kuwapasha Wananchi yanayojiri katika Uendeshaji bora wa Shughuli za Bunge. Dhamira ya Bunge ni kuhakikisha kuwa mpango kabambe uliopo ni kumfikia kila Mtanzania alipo na kwa uwezo alionao aweze kupata na kushiriki katika uendeshaji wa shughuli za Bunge.
Hivyo Mpango mkakati uliopo utakuwakuboresha mawasiliano ya kawaida kupitia Teknolojia ya Mawasiliano TEKNOHAMA, kwa wale watakaokuwa na uwezo wa kupata huduma za mtandao, na tayari tumeanza kurusha live video striping kupitia tovutiya Bunge, na hata wale watakaopenda kujua zaidi, basi wanaweza kupitia majadiliano ya Bunge kwa nyakati tofauti. Aidha, kwa wale watakaokuwa na uwezo wa kushika mawimbi ya Radio, basi wataweza kufuatilia majadiliano ya Bunge katika Radio ya Bunge inayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni katika masafa yanayoweza kupatikana nchi nzima, hii ikiwa ni jitihada za ziada kwa kuwa kunaRadio zinazotoa huduma hiyo ya moja kwa moja vizuri hadi sasa, kama vile RTD,BBC, STAR etc. Aidha, kwa wale watakaoweza kuwa na uwezo wa kumudu Luninga, basi Bunge limejipanga kuwapatia huduma hiyo moja kwamoja kupitia katika mtandao wake mpya utakaokuwa ukirushwa masaa 24, baada ya mitambo mipya ya kunakili majadiliano Bungeni na katika Kamati kusimikwa.
Hivyo basi utaratibu uliopo sasa utaendeleakutumika ambapo vituo vyote vya Television vitapewa fursa ya kurusha matangazokwa utashi wao bila kuwekewa mipaka ya aina yoyote sambamba na matangazoyatakayotolewa na mitandao ya Bunge. Utaratibu huu unatokana na uamzi wapamoja kati ya Bunge na Tume ya Mawasiliano, ambapo vipindi vyote vya Bungevitakuwa vinarushwa bila kudhaminiwa na taasisi yoyote zaidi ya mamlaka tajwajuu ya mawasiliano TCRA. Hivyo basi kwa maelezo hayo ni dhahirikwua Bunge halina mpango wa kusitisha matangazo ya TV wala yale ya Radio auTecknohama, bali linatarajia kuboreshaupatikanaji wa huduma kwa utaratibu ulio rahisi na unaoweza kusimamiwa na pandezote, yaani Bunge na Wananchi.
Aidha, kwa utaratibu uliopo sasa,Bunge halirushi matangazo ya aina yoyote, bali hutoa nakala ya majadiliano hayokwa mtu yeyote atakaye au TV na Radio yoyote kupitia katika mitambo yake. TV zote zinazorusha matangazo ya Bunge hupatafeedtoka katika mitambo ya Bunge, napale wanapoona yafaa basi huomba kutumia mitambo yao na hivyo kutumia fursahiyo kuingiza Camera na Wanahabari ndani ya kambi la Bunge kwa minajirihiyo.
Kuzingatia mabadiliko tajwa, utaratibuhuo umepewa ukomo, ili sasa hapatakuwa na fursa ya kuingiza Camera ndani yaKumbi za Bunge, bali wote watakaotaka kurusha matangazo ya Bunge kwa utashiwao, watapata clear feed toka katikamitambo ya Bunge na hivyo kurusha livevipindi vyote vya Bunge bila kuhaririwa kama ilivyonakiliwa katika makala mbalimbali. Hata hivyo utaratibu huu wa kutumia Camerakatika Kumbi utaendelea katika Kamati za Bunge, hadi hapo mitambo mipya ya mawasilianoitakapofungwa katika Kumbi zote za Kamati. Hivyo basi, ili kwenda sawia nataratibu hizo, Bunge litaendesha zoezi la kuwatathmini Waandishi wote wa habariza Bunge na kuwasajili kwa vigezo vitakavyoafikiwa kati ya Baraza la Habari,Idara ya Habari na Bunge lenyewe.
Aidha ili kulinda heshima na maadiliya utangazaji, Bunge litatoa utaratibu (Codeof Conducts for Media broadcasting) wa namna ya kunakili na kurushamatangazo ya Bunge bila kujali yanarushwa kwa utaratibu upi. Hili litasaidia kuweka misingi bora yamawasilaino na hivyo kuwapa fursa Wananchi kujua hali halisi ya matukio yotendani ya Bunge na katika Kamati, bila kuegemea upande wowote (Non Partisan).
Hivyo basi, wakati zoezi la maboreshohayo likiendelea, Wananchi watajulishwa kila hatua na matarajio tajwa na kwambatunaendelea kusisitiza tena, Wananchiwasiwe na hofu juu ya taarifa zilizopewa uzito usio stahili za kusitishamatangazo ya Bunge, ambao hazikuwa sahihi na pia hazikuainisha zoezi zima lamaboresho ya upatikanaji na usambazaji wa habari za Bunge.
Tunasikitika kwa usumbufu uliowasibuwote walioakisiwa na taarifa hiyo.
Dr. Thomas D.Kashililah
KATIBU WA BUNGE